Mwanachuo kutoka Chuo cha Mzumbe,ambaye ni mshindi wa vifaa vya nyumbani katika kampeni inayoendelea ya Magifti Dabo Dabo, Ayoub Mwenda akipokea vifaa hivo kutoka kwa Meneja wa Tigo kanda ya Pwani, Gwamaka Mwakilembe, pembeni ni mshindi mwenza, Selemani Omary.
Na Mwandishi Wetu.
Mwanachuo kutoka Mzumbe Mkoani Morogoro Ayoub Mwenda ameshinda Vifaa vya Nyumbani ambavyo ni Friji , TV , Microwave na Sound bar kutokana na Kampeni inayoendelea hivi sasa ya Magifti Dabo Dabo na kumchagua rafiki yake Seleman Omary kuwa mshindi mwenza ambaye naye amepewa Vifaa ivyo ivyo ili kuleta maana halisi ya Kampeni hii MAGIFTI DABO DABO ambapo ukishinda na mwenzako anashinda .
Ikumbukwe Kampeni hii inayoendeshwa na Kampuni ya Tigo imezinduliwa wiki kadhaa zilizopita huku ikimtambulisha Haji Manara kama SEMAJI la Kampeni hii, ambapo mteja wa Tigo anaweza kushinda Fedha Taslimu hadi Milioni 10, Safari ya Kwenda Dubai au Zanzibar, Set ya Vifaa vya Ndani ambavyo ni Sound bar, Friji, TV na Microwave na Zawadi kubwa ya Magari Mawili ( 0km ) , kingine kinachovutia katika kampeni hii ni kwamba ukishinda kitu kimoja wapo kati ya ivyo unamchagua na yeyote umpendae ili apewe zawadi iyoiyo uliyoshinda hii ndio maana halisi ya MAGIFTI DABO DABO.
Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa ivyo , Meneja wa Tigo kanda ya Pwani, Gwamaka Mwakilembe amewasisitiza Wanachuo na Watanzania kufanya miamala mbalimbali na Tigo Pesa ili kuibuka washindi maana kampeni bado inaendelea
" Muda huu tunaozungumza kuna washindi 15 wametoka DUBAI kula " BATA " wengine wametoka Zanzibar kuna wengine wamejishindia Pesa Taslimu na wapo pia wamejishindia Vifaa vya Hisense kama hawa tunaowashuhudia, kampeni bado inaendelea fanyeni miamala na TIGO PESA kwa wingi, Lipa kwa Simu, nunua vifurushi ili utengeneze mazingira ya kuibuka Mshindi " alisema Mwakilembe
No comments: