Header Ads Widget

Recent in Sports

test

TBS YAWATAKA WADAU KUSHIRIKI KWENYE UANDAAJI WA VIWANGO , KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA VIWANGO

 Na Mwandishi Wetu.

Katika kuadhimisha Siku ya Viwango Duniani, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewataka wadau na wananchi kushiriki vyema katika uandaaji wa viwango ili kwa pamoja tuweze kuandaa viwango vinavyotekelezeka .

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Oktoba 13,2023 Jijini Dar es Salaam, Meneja wa Viwango Bw.Yona Afrika amesema kuna umuhimu mkubwa wa wadau kushiriki katika uandaaji wa viwango kwani viwango vinasaidia uzalishaji wa bidhaa bora nchini na kuweza masoko makubwa ndani na nje ya nchi.

Aidha amesema kuwa viwango vinasaidia kupunguza gharama pamoja na kukuongezea wateja kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi.

Amesema suala la uandaaji wa viwango linahusisha wadau wote wa uzalishaji wa bidhaa na sio la Shirika la Viwango pekee.

Siku ya Viwango Duniani huadhimishwa kila ifikapo Oktoba 14 kila mwaka


TBS YAWATAKA WADAU KUSHIRIKI KWENYE UANDAAJI WA VIWANGO , KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA VIWANGO TBS YAWATAKA WADAU KUSHIRIKI KWENYE UANDAAJI WA VIWANGO , KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA VIWANGO Reviewed by Adery Masta on October 13, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.