Ijumaa ya Oktoba, 13 , 2023 Shirika la Air France la nchini Ufaransa limesheherekea miaka 90 ya utoaji Huduma Za Usafiri wa Anga Duniani kote.
Ikumbukwe Shirika hili lilirudi Ndani Ya Tanzania na kuendelea kutoa huduma ya Usafiri wa anga Mnamo Oktoba 2021 likianzia Zanzibar - Ufaransa na hatimae mnamo Juni Mwaka huu lilizindua safari nyingine tena ya Dar Es Salaam - Paris Ufaransa.
Akizungumzia Miaka 90 ya AIR FRANCE Meneja Mkuu wa Air France - KLM kwa Afrika Mashariki Kusini, Nigeria na Ghana Bwn. Marius Van der Ham amesema
" Katika kusheherekea miaka 90 tunachojivunia ni ukuaji, Ukuaji katika kukuza matawi ya Utoaji wa Huduma zetu katika nchi mbalimbali hapa duniani, tunachokipambania siku zote ni kutimiza takwa la kila mteja wetu na ndio maana ndege Zetu zina kila hitaji ambalo Mteja wetu anastahili kupewa, na hilo ndo linatufanya tuendelee kuwa kileleni siku zote huku tukiwafanya watu wajivunie utamaduni ya Kifaransa, Nikizungumzia AIR FRANCE ndani ya Afrika Mashariki, tukirudi Nyuma miaka mitano iliyopita haikuwepo , kwahiyo ujio wetu mpya ndani ya Afrika Mashariki hasahasa Ndani Ya nchi ya Tanzania umeleta manufaa makubwa kwa Tanzania na Ufaransa, na kuimarisha uhusiano wa kiutamaduni na kiuchumi kati ya nchi Zetu mbili inabidi tusherekee kwa hilo " amesema Van Der HamNaye Mwenyekiti Wa Wakala wa Tiketi za Ndege Tanzania Bi. Agnes Rwegasira akiizungumzia Miaka 90 ya Shirika la Ndege la Air France amesema Shirika hili linajinasibu kwa Ufahari kwasababu ni Shirika ambalo linajivunia kutoa huduma bora
" Mimi ni Msafiri mzuri wa ndege zao na wana Mambo mazuri yasiyosimulika " ELEGANCE " katika Vyakula, Huduma zao kwenye Ndege, viti vyao, Wahudumu wao n.k " alimalizia Bi. Rwegasira.
No comments: