Header Ads Widget

Recent in Sports

test

MBUNGE KANYASU AWAPIGIA " SALUTE " BRELA , MAONESHO YA SITA YA MADINI GEITA

                              

Mbunge wa Jimbo la Geita Mhe. Constantine Kanyasu ( Kushoto ) akipokea maelezo kuhusu majukumu ya BRELA kutoka kwa Mkuu wa Sehemu ya Majina ya Biashara Bw. Harvey Godwin Kombe ( Kulia ) mara baada ya kutembelea banda la BRELA katika maonesho ya Sita ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya EPZA - GEITA.

***************
Na Mwandishi Wetu.

MBUNGE wa Jimbo la Geita Mhe. Constantine Kanyasu amewapongeza Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kwa kuendelea kutoa Elimu kwa wadau kikamilifu Kwa wananchi mbalimbali ambao wamekuwa wakitembelea kwenye banda lao kwa lengo la kujua majukumu ya taasisi hiyo.

Kanyasu amebainisha hayo leo Septemba 26, 2023 Mkoani Geita mara baada ya kutembelea kwenye banda la Brela lililopo kwenye Maonesho ya Sita ya  ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini chini ya kauli mbiu " Matumizi ya Teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi Mazingira"  yanayofanyika katika viwanja vya EPZA Bombambili Halmashauri ya Mji Geita

Naye Mkuu wa Sehemu ya Majina ya Biashara (Brela) Bw. Harvey Godwin Kombe akimueleza majukumu ya Brela Mbunge wa Jimbo la Geita Mheshimiwa Constantine Kanyasu mara baada ya kutembelea banda lao katika Maonesho ya Sita ya Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya EPZA Halmashauri ya Mji wa Geita Leo Septemba 26, 2023.



.

MBUNGE KANYASU AWAPIGIA " SALUTE " BRELA , MAONESHO YA SITA YA MADINI GEITA MBUNGE KANYASU AWAPIGIA " SALUTE " BRELA , MAONESHO YA SITA YA MADINI GEITA Reviewed by Adery Masta on September 29, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.