Header Ads Widget

Recent in Sports

test

TIGO CHA WOTE YAMWEZESHA MHITIMU WA CHUO KUTIMIZA NDOTO YAKE

 Na Mwandishi Wetu. 

Joyce Nestor Masaba , Mhitimu wa Chuo Mkazi wa Mbezi Beach Jijini Dar Es Salaam ni miongoni mwa washindi wa Milioni Moja ambaye anaenda kutimiza ndoto yake Ya kumiliki biashara yake mwenyewe kutokana na ushindi aloupata kupitia Kampeni ya Tigo CHA WOTE wiki ya Nane ambapo hadi sasa Tigo wameshatoa Fedha Taslim na zawadi mbalimbali kwa Washindi zaidi ya elfu 17 Nchi Nzima tangu kampeni hii izinduliwe. 



Akizungumza Leo Agosti 18 , 2023. Wakati wa Kuwakabidhi Mfano wa Hundi Baadhi ya Washindi wa Milioni Moja Moja wiki ya nane waliobahatika kufika Tigo Makao Makuu, Meneja Wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi Mary Rutha amesema kuwa hadi sasa ikiwa ni wiki Nane tu tangu Kampeni iyo izinduliwe wameshapatikana washindi zaidi ya elfu 17 kutoka maeneo mbalimbali nchini .

" Leo tunayo furaha kubwa kuwa na baadhi ya washindi wa Wiki ya Nane wa Kampeni  ya TIGO CHA WOTE ambao hawa ni washindi wa Milioni Moja Moja kila mmoja, Lakini niwakumbushe Watanzania kwamba kila siku CHA WOTE inatoa zawadi ikiwemo pesa taslimu hadi Milioni Moja kwa washindi 320 kila siku , kuibuka mshindi ni rahisi tu unachotakiwa ni kufanya miamala na Tigo Pesa kama Kutumia Lipa Kwa Simu , Kununua Vifurushi , Kulipia Bili kwa Tigo Pesa , n.k kwa kufanya ivyo nawewe siku si nyingi utakua miongoni mwa Washindi wa Kampeni hii ya CHA WOTE ".  maana bado washindi zaidi ya elfu 10 wanatafutwa" Alisema Bi. Mary Rutha 

Nae Amina Rajabu Mkazi wa Dar es salaam mshindi wa milioni moja ameongezea kwa kusema   fedha hiyo itamsaidia kwenye biashara yake ya mama lishe  kuongezea mtaji wake na kukuza biashara hiyo.

Sanjari na hayo Mshindi mwingine wa milioni Moja Godfrey Tarimo mkazi wa Dar es Salaam amesema  hela hiyo itamsaidia katika mambo yake mengine binafsi.

TIGO CHA WOTE YAMWEZESHA MHITIMU WA CHUO KUTIMIZA NDOTO YAKE TIGO CHA WOTE YAMWEZESHA MHITIMU WA CHUO KUTIMIZA NDOTO YAKE Reviewed by Adery Masta on August 18, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.