Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linaendelea na Kampeni yake Ya kutoa Elimu Kwa Umma katika Ngazi za Wilaya ambapo hadi sasa Shirika hilo limetoa Elimu Kwa wananchi Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wadogo Ndani ya Wilaya 63 nchi nzima na Lengo likiwa ni kuzifikia Wilaya Zote nchini.
Akizungumza Leo Agosti 21, 2023 katika Wilaya Ya Malinyi mkoani Morogoro Meneja Wa Uhusiano na Masoko TBS Bi. Gladnes Kaseka amesema lengo la Shirika hilo ni kutoa Elimu Kwa Umma katika Ngazi za Wilaya zote.
" Kwa sasa TBS tumeamua kuwafikia Wajasiriamali ,Wafanyabiashara na wananchi katika Ngazi Za Wilaya ili kuwapatia utaratibu unaotakiwa kwa ajili ya kupata alama ya Ubora na kusajili majengo ya Biashara ya chakula na Vipodozi ili kuepuka Usumbufu unaoweza kujitokeza kwahiyo Elimu hii ya Umma ipo katika ngazi ya Wilaya na hadi sasa TBS imezifikia Wilaya 63 , Leo tupo hapa Malinyi vilevile tutaendelea na wilaya ya Ulanga, Gairo na Mvomero katika Mkoa huu wa Morogoro ". amesema Bi. Kaseka
Nao Wajasiriamali kutoka vijiji mbalimbali vya Wilaya Ya Malinyi wamelipongeza Shirika la Viwango Tanzania Kwa Elimu waliyoamua kutoa kwa maana imewafumbua Mambo mengi kuhusu umuhimu wa Viwango katika bidhaa wanazozizalisha.
No comments: