"Niwakaribishe wote katika Kongamano la Uwekezaji katika sekta ya Madini yaani " Mining & Investment Forum 2023" na niwahakikishie kwa mwaka huu litakua la kitofauti sana , tunategemea kupokea wageni zaidi ya 2000 kutoka kote duniani na tunataka kufungamanisha sekta ya Madini na Sekta ya Utalii kwa maana wale watakao kuja kwenye kongamano hili washafanya Booking kutembelea vivutio vyetu hapa nchini "
Hayo yamesemwa leo Mei 23,2023 Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Madini Dotto Biteko, kwenye Mkutano na Waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa Kongamano la Uwekezaji katika Sekta ya Madini mwaka 2023, lijulikanalo kama Tanzania ‘Mining & Investiment Forum 2023′ litakalofanyika Octoba 25 hadi 26, Mwaka huu.
Amesema kuwa mkutano huo utahusisha wadau kutoka Mataifa mbalimbali Duniani, lengo ni kujadili masuala mbalimbali ya ukuzaji Sekta ya madini.
Dkt. Biteko ameeleza kuwa Mkutano huo, huwa ukifanyika mwezi Februari kila mwaka tangu mwaka 2020, lakini kwa mwaka huu wamebadilisha kutokana na tarehe hiyo kuwa na majukumu mengine yaliyofanyika katika Mataifa mengine ambapo Tanzania ilishiriki.
“Tumefanya mabadiliko ya tarehe ambapo utafanyika kwa siku mbili Octoba 25 na 26, na utakuwa na utofauti na mikutano mingine ambao unaleta wazungumzaji wengi zaidi kuliko miaka iliopita, na mada zitakazozungumzwa ni nyingi zaidi kuliko miaka mingine.
“Utakuwa na wageni kutoka Serikalini, tutawaalika Mawaziri mbalimbali ambao watakuja. Makampuni makubwa ya uchimbaji Duniani watakuja, wachimbaji wakubwa kutoka Duniani watakuja, lakini wataalamu na watafiti mbalimbali watakuwa pamoja nasi.
“Kwa hiyo utakuwa ni mkutano mkubwa ambao utakuwa ni wakujadili mwaswala ya ukuzaji wa Sekta ya Madini kuangalia nanma gani Sekta hii inaweza kuwanufaisha watu na kuwatoa katika umaskini” ameeleza Dkt. Biteko.
Aidha Dkt. Biteko amewakaribisha watu mbalimbali kushiriki pamoja nao kwenye mkutano huo, nakwamba Tanzania imejipanga kikamilifu kuhakikisha mkutano huo unakwenda vizuri na kufika malengo yake.“Nitoe wito kuwa mkutano huu utakuwa ni wa kipekee na wa aina yake, tunataka kufunganisha Sekta ya Madini na Utalii kwaajili ya mkutano huu, kutakuwa na wageni mbalimbali kutoka nchi mbalimbali Duniani kwenye mkutano huu, wameshatoa oda kwenda kwenye mbuga za wanyama na Zanzibar kwa ajili ya utalii, hivyo hii ni fursa”amesema Dkt.Biteko.
Naye kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Maji . Nishati na Madini Zanzibar Bwn. Joseph Kilanga amesema Mkutano huu utaongeza watalii na kuongeza ushirikiano baina ya Tanzania na Zanzibar na kuongezea kuwa Serikali ya Zanzibar ipo tayari kuwapokea watalii hao.
No comments: