Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe. Abbas Tarimba akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma ya maji safi na salama ya HERITAGE DRINKING WATER ndani ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii ( Institute of Social Work ) Iliyopo Sinza Bamaga Jijini Dar Es Salaam.
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe. Abbas Tarimba akitoa neno mda mchache kabla ya uzinduzi rasmi wa huduma ya maji safi na salama ya HERITAGE DRINKING WATER ndani ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii ( Institute of Social Work ) .
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe. Abbas Tarimba akimpongeza Naibu Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Sotco Komba kwa kukubali kuipokea huduma ya maji safi na salama ya HERITAGE DRINKING WATER , na kumsihi kutunza huduma hii kutoka kwa Mwanzilishi ambaye ni mzawa kushoto ni Dkt. Edwinus Lyaya Mkurugenzi mtendaji wa Heritage Drinking Water.
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe. Abbas Tarimba akipongeza baada ya kupokea maelekezo ya jinsi mashine hizi za maji safi na salama ya HERITAGE DRINKING WATER zinavyofanya kazi .
Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya HERITAGE DRINKING WATER katika picha ya pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe. Abbas Tarimba mda mchache baada ya Uzinduzi wa huduma ya Maji ndani ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii ( Institute of Social Work ) Iliyopo Sinza Bamaga Jijini Dar Es Salaam.
...................................................................*****************........................................................
Na Mwandishi Wetu.
Kampuni ya Kitanzania ya Uuzaji wa maji safi na Salama kwa bei nafuu ya Tsh. 200 / Litre ya HERITAGE DRINKING WATER Leo Agosti 17, 2022 imefungua kituo kipya cha kuuza maji ndani ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii ( Institute of Social Work ) Iliyopo Sinza Bamaga Jijini Dar Es Salaam kituo kilichozinduliwa rasmi na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe. Abbas Tarimba
Akizungumza kabla ya Uzinduzi huo Mhe. Tarimba amempongeza Bwn. Edwinus Lyaya ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa Heritage Drinking Water , kwa Ubunifu huu na kuahidi kuunga mkono kampuni hii ya Kitanzania kuhakikisha inaendelea kutoa huduma hii ya Maji safi na salama ambaye kauli mbiu yake ni " TUNZA PESA OKOA MAZINGIRA "
" Hakika HERITAGE DRINKING WATER mnafanya mambo makubwa na hatuna budi kuwaunga mkono , nimeona hapa bei za maji yenu Shilingi 200 kwa lita moja ni bei ndogo sana kulinganisha na ubora wa maji mnayoyatoa hakika inabdi tuwaunge mkono muweze kuwafikia watanzania wengi zaidi Ndani na hata nje ya Jiji la Dar Es Salaam ili kila mtanzania aweze kuokoa pesa huku akitunza mazingira kama kauli mbiu yenu inavyosema " Alimalizia Mhe. Tarimba.
Naye kwa upande wake Naibu Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Sotco Komba ameipongeza na kuiahidi Kampuni ya HERITAGE DRINKING WATER kuwa kama uongozi wa Taasisi watahakikisha wanatunza miundo mbinu hiyo ya maji maana imekuwa mkombozi ndani ya Taasisi hiyo na hata kwa watu walioko maeneo jirani.
No comments: