Afisa Mkuu wa Tigo Pesa Bi. Angelica Pesha ( aliyesimama ) akizungumza na baadhi ya wanawake wafanyabiashara na Wajasiriamali zaidi ya 35 wa Soko la Kariakoo Jijini Dar Es Salaam Jana Agosti , 11 , 2024 kikao kilichowakutanisha Tigo na wafanyabiashara wanawake wa kariakoo ikiwa ni mkakati mkubwa wa Tigo kuhakikisha wanaunga mkono wanawake kukua kibiashara kupitia huduma za Tigo.
Na Adery Masta.
Jana Agosti 11, 2024 Kampuni ya utoaji wa Huduma za Mawasiliano ya Tigo ilifanya kikao maalum na Wanawake wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo Jijini Dar Es Salaam kwa lengo la kuhakikisha wanaunga mkono jitihada za Wanawake hasa Wafanya biashara na Wajasiriamali wote , kuwapa uelewa wa namna ya kutunza kumbukumbu za fedha na mahesabu, lakini pia watatumia mtandao wa tigo katika kufanya miamala kidigital hasa kupitia lipa namba na huduma zingine zinazomfanya mfanyabiashara afanye malipo bila kuwa na pesa taslimu.
Akizungumza baada ya Mkutano huo , Afisa Mkuu wa Tigo Pesa Bi. Angelica Pesha amesema Mkutano huo umetoa elimu na manufaa ya huduma mbalimbali za tigo kwa wafanyabiashara wanawake wa kariakoo (kariakoo business women ) ikiwa ni pamoja na huduma ya lipa kwa simu ambayo inasaidia kutunza kumbukumbu na kuwa na miamala ya kidigitali.Aidha amesema kuwa mkutano huu umesaidia kuona ni changamoto gani wafanyabiashara wanawake wa kariakoo wanazozipitia ambazo watazifanyia kazi kwa kupanga mpango mkakati mfupi na mrefu ili kuwawezesha wanawake waweze kufanya biashara kiurahisi na salama kupitia Tigo pesa ili kufikia uchumi wa kidigitali na kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha inachangia ujumuishwaji wa kifedha kwa wananchi kupitia huduma zake za kifedha kwa njia ya digitali , Angelica amefafanua kuwa Juhudi hizi ni moja ya mkakati wa kuunga mkono serikali ya kuhakikisha wanafikia makundi mbalimbali ikiwemo wanawake lakini pia kufikia uchumi jumuishi, hivyo tigo imetenga muda wake kuweza kuwasikiliza na kuona ni suluhisho zipi wanazoweza kutoa katika huduma zake kwa ajili ya biashara ambayo itakua na tija kwa mfanyabiashara hasa za kidigitali.Akizungumza kwa niaba ya wanawake hao Bi. Fransiska Limo amesema kuwa tigo wamekuja kufungua akili yao, wamepata elimu ya uelewa wa namna ya kutunza kumbukumbu za fedha na mahesabu, lakini pia watatumia mtandao wa tigo katika kufanya miamala kidigital hasa kupitia lipa namba na huduma zingine zinazomfanya mfanyabiashara afanye malipo bila kuwa na pesa taslimu.
TIGO WATOA ELIMU YA FEDHA KWA WANAWAKE KARIAKOO
Reviewed by Adery Masta
on
August 12, 2024
Rating:
No comments: