Clement Mahemba Mkazi wa Ubungo Jijini Dar Es Salaam akijaribu viatu baada ya kuvinunua katika Banda la DIT lililopo Maonesho ya Sabasaba , kulia ni Mtaalam wa Uchakataji wa Bidhaa za Ngozi kutoka DIT Kampasi ya Mwanza Ramadhan Khalfan Buthu.
Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam ( DIT ) inashiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Temeke Jijini Dar Es Salaam , na DIT imekuja na Bunifu mbalimbali zilizobuniwa na Wanafunzi wa Taasisi hiyo nyingine zikitoka kwenye Kampuni Tanzu ya Taasisi hiyo maarufu kama DIT COMPANY.
Bidhaa zilizowavutia watu wengi waliotembelea Banda la DIT ni bidhaa za Ngozi kama vile Viatu, mikanda n k ambazo zinatengenezwa na DIT Kampasi ya Mwanza .
Clement Mahemba Mkazi wa Ubungo Dar Es Salaam ni miongoni mwa watu waliopata bahati ya kutembelea Banda la DIT Leo Julai 04 , 2024 na kununua viatu akizungumza na Mwandishi Wetu na kuulizwa kwanini ameamua kununua viatu vya DIT Clement amesema kwamba sababu kuu ni BEI na UBORA.
" Nimekua nkisikia kuhusu bidhaa za Ngozi za DIT hasa hasa Viatu na Mikanda na baada ya kufika katika Maonesho haya nikaona wana Banda lao ndipo nikaingia na kununua pea kadhaa za Viatu , kwakweli viatu vyao ni vigumu (Ngozi asilia ) na Bei nafuu ". amesema
Aidha Clement amewasihi Wazazi na Vijana hasa waliomaliza kidato cha 4 na 6 waweze kujiunga na DIT Kampasi ya Mwanza ili kujipatia ujuzi wa Kutengeneza bidhaa kama hizi maana itawapa mwanya mpana wa kujiajiri na kuajirika katika makampuni mbalimbali na hata Serikalini.
No comments: