Na Mwandishi Wetu.
Wizara ya Afya Zanzibar, imeitaka kampuni ya simu ya mkononi Tigo Zantel na Laina Finance Limited kuangalia uwezekano mwengine wa kurahisha huduma za upatikanaji wa bidhaa mbalimbali kwa wateja wao hasa wakati wa dharura.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Hassan Khamis Hafidh, ameeleza hayo wakati akizindua huduma ya Pata Dawa kupitia simu ya Mkononi Tigo Zantel kwa kushirikiana na Laina Finance Limited .
Ameipongeza Tigo Zantel na Laina Finance kuja na program hiyo ya PATA DAWA ambayo itamuwezesha mtumiaji wa mtandao huo kupata huduma za dawa kwa njia ya mkopo na kurudisha fedha hizo kwa kipindi cha siku kumi na kuwatka pia kubuni huduma nyengine mbalimbali ambazo zitaweza kuwasaidia wateja wao hasa katika kipindi cha dharura.
Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Tigopesa, Angelica Pesha amesema kampuni hiyo inatengeneza historia kwani huduma ya PATA DAWA ni huduma ya kidijitali na Tanzania ndo nchi pekee yenye huduma hii ndani ya Afrika Mashariki.
Amesema tayari wameshasajili maduka ya dawa na hospitali mbalimbali kwa Unguja na Pemba na mteja akienda katika maduka hayo na amepata dharura na hana uwezo wa fedha katika akaunti yake ya tigo pesa basi anaweza kuhudumiwa kupitia huduma hiyo ya PATA DAWA NA TIGO PESA.
Naye Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Saleh Omar Kaabi, ameipongeza kampuni hiyo kuja na jambo hilo ambalo halina riba kwa kufata misingi sahihi ya dini ya kiislamu
No comments: