Header Ads Widget

Recent in Sports

test

NI RAHISI KUIBUKA MSHINDI WA MAGIFTI DABO DABO YA TIGO , FANYA MIAMALA NA TIGO PESA

 Na Mwandishi Wetu

Januari 19, 2024 Farida Keppy Kyeumbile na Mohammed Salum ni baadhi ya Wawakilishi wachache kutoka Dar Es Salaam waliojishindia Milioni Moja Moja na kuingia kwenye Orodha ya zaidi ya Washindi 100 wa kampeni ya MAGIFTI DABO DABO inayoendelea hivi sasa.

Ikumbukwe Kampeni hii inayoendeshwa na Kampuni ya Tigo ilizinduliwa Mwishoni mwa Mwezi Novemba Mwaka jana huku  ikimtambulisha Haji Manara kama SEMAJI la Kampeni hii, ambapo mteja wa Tigo anaweza kushinda Fedha Taslimu hadi Milioni 10, Safari ya Kwenda Dubai au Zanzibar, Set ya Vifaa vya Ndani ambavyo ni Sound bar, Friji, TV na Microwave na Zawadi kubwa ya Magari Mawili ( 0km ) , kingine kinachovutia katika kampeni hii ni kwamba ukishinda kitu kimoja wapo kati ya ivyo unamchagua na yeyote umpendae ili apewe zawadi iyoiyo uliyoshinda hii ndio maana halisi ya MAGIFTI DABO DABO.

Akizungumza baada ya kuwakabidhi washindi mfano wa Hundi Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi. Mary Rutha  amewasisitiza  Watanzania kufanya miamala mbalimbali na Tigo Pesa ili kuibuka washindi wa Pesa Taslimu, Vifaa vya Hisense na Zawadi kubwa ya Magari Mawili katika Droo Tatu Zilizobakia.


" Mwezi Disemba Tigo tuliwapeleka washindi 15  DUBAI , na wengine walienda Zanzibar katika kampeni hii hii" wapo pia waliojishindia Pesa Taslimu na wapo pia wamejishindia Vifaa vya Hisense. kwahyo kampeni bado inaendelea fanyeni miamala na TIGO PESA kwa wingi, Lipa kwa Simu, nunua vifurushi ili utengeneze mazingira ya kuibuka Mshindi " amesema Mary Rutha .

NI RAHISI KUIBUKA MSHINDI WA MAGIFTI DABO DABO YA TIGO , FANYA MIAMALA NA TIGO PESA NI RAHISI KUIBUKA MSHINDI WA MAGIFTI DABO DABO YA TIGO , FANYA MIAMALA NA TIGO PESA Reviewed by Adery Masta on January 19, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.