Na Mwandishi Wetu.
Disemba 14, 2023 Bi . Rehema Makunganya Mkazi wa Mbezi Kimara anayefanya biashara ya Mama Lishe katika Soko la Mapinduzi Mwananyamala Jijini Dar Es Salaam anaenda kutimiza ndoto yake ya kufungua mgahawa mkubwa baada ya kushinda na kukabidhiwa rasmi Milioni 10 kutoka kampeni ya MAGIFTI DABO DABO inayoendelea hivi sasa.
Meneja wa Tigo Kanda ya Dar Es Salaam , Beatrice Kinabo akimkabidhi mfano wa Hundi ya Shilingi Milioni 10 Mshindi wa Promosheni ya MAGIFTI DABO DABO Mama Lishe, mkaazi wa Mbezi Kimara Bi. Rehema Makunganya.Ikumbukwe Kampeni hii inayoendeshwa na Kampuni ya Tigo imezinduliwa wiki kadhaa zilizopita huku ikimtambulisha Haji Manara kama SEMAJI la Kampeni hii, ambapo mteja wa Tigo anaweza kushinda Fedha Taslimu hadi Milioni 10, Safari ya Kwenda Dubai au Zanzibar, Set ya Vifaa vya Ndani ambavyo ni Sound bar, Friji, TV na Microwave na Zawadi kubwa ya Magari Mawili ( 0km ) , kingine kinachovutia katika kampeni hii ni kwamba ukishinda kitu kimoja wapo kati ya ivyo unamchagua na yeyote umpendae ili apewe zawadi iyoiyo uliyoshinda hii ndio maana halisi ya MAGIFTI DABO DABO.
Akizungumza baada ya kumkabidhi Hundi ya Milioni 10 Mshindi , Meneja wa Tigo Kanda ya Dar Es Salaam Bi. Beatrice Kinabo amewasisitiza wafanyabiashara wa Mwananyamala na Watanzania kufanya miamala mbalimbali na Tigo Pesa ili kuibuka washindi maana kampeni bado inaendelea
" Muda huu tunaozungumza kuna washindi 15 wapo DUBAI wanakula " BATA " wengine wapo Zanzibar kuna wengine wamejishindia Pesa Taslimu na wapo pia wamejishindia Vifaa vya Hisense kwahyo kampeni bado inaendelea fanyeni miamala na TIGO PESA kwa wingi, Lipa kwa Simu, nunua vifurushi ili utengeneze mazingira ya kuibuka Mshindi " alisema Beatrice
Akizungumza kwa furaha kubwa, Mshindi wa Milioni 10 Bi Rehema Makunganya amesema kwakweli haamini macho yake kama tukio lililokua linafanyika ni la kwelii,
" Mara ya kwanza napigiwa simu kuambiwa nimeshinda Milioni 10 ya MAGIFTI DABO DABO sikuamini kwakweli, Nilijua ni utapeli lakini baadae nkaja kuamini baada ya kuona kumbe nimepigiwa na namba 100 nawasihi Watanzania tumieni Tigo, fanyeni miamala maana ndo Siri ya Ushindi, nilikua na Genge lakini sasa naenda kufungua mgahawa mkubwa " alisema Bi Rehema kwa furaha kubwa.
No comments: