.
Afisa Usalama wa Chakula TBS Bwn. Barnabas Jacob na Afisa Masoko Mussa Luhombero wakitoa Elimu kwa wazalishaji wadogo wadogo wa bidhaa mbalimbali katika Mkoa wa Mtwara , kuhusu umuhimu wa kuwa na alama ya ubora kutoka TBS ambayo inatolewa BURE.
Afisa Masoko TBS Bi. Rhoda Mayugu akizungumza na wafanyabiashara wa Mkoa wa Mtwara kuhusu kuhakikisha wanauza bidhaa zenye alama ya Ubora kutoka TBS , na kuhakikisha wanazingatia kikomo cha muda wa matumizi ya bidhaa ( EXPIARY DATE )ili kuepukana na kuwauzia wateja wao bidhaa zinazoweza kuwaletea madhara , au bidhaa hizo kuharibiwa pale zitakapogundulika.
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linaendelea na Kampeni yake Ya kutoa Elimu Kwa Umma katika Ngazi za Wilaya ambapo hadi sasa Shirika hilo limetoa Elimu Kwa wananchi, Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wadogo kwa zaidi ya Wilaya 76 nchi nzima na Lengo likiwa ni kuzifikia Wilaya Zote nchini.
Akizungumza hapo jana Oktoba 16 , 2023 katika Halmashauri ya manispaa ya Mikindani Mkoani Mtwara Afisa Masoko TBS Bw. Mussa Luhombero amesema lengo la Shirika hilo ni kutoa Elimu Kwa Umma katika Ngazi za Wilaya zote.
" Kwa sasa TBS tumeamua kuwafikia Wajasiriamali ,Wafanyabiashara na wananchi katika Ngazi Za Wilaya ili kuwapatia utaratibu unaotakiwa kwa ajili ya kupata alama ya Ubora na kusajili majengo ya Biashara ya chakula na Vipodozi ili kuepuka Usumbufu unaoweza kujitokeza kwahiyo Elimu hii ya Umma ipo katika ngazi ya Wilaya na hadi sasa TBS imezifikia zaidi ya wilaya 76 nchi nzima , Leo tupo hapa Halmashauri ya Manispaa Mtwara - Mikindani vilevile tutaendelea katika wilaya ya Tandahimba, Newala, Nayumbu na Masasi katika Mkoa huu wa Mtwara ". amesema Bwn. MussaNao Wazalishaji wa bidhaa , Wananchi na Wajasiriamali wadogo wadogo kutoka maeneo mbalimbali ya Mikindani wamelipongeza Shirika la Viwango Tanzania Kwa Elimu waliyoamua kutoa kwa maana imewafumbua Mambo mengi kuhusu umuhimu wa Viwango katika bidhaa wanazozizalisha na kuzitumia.
No comments: