SERIKALI YA ZANZIBAR NA TIGO ZANTEL WASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO KUPELEKA HUDUMA ZA INTANETI MAJUMBANI
Na Mwandishi Wetu.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia shirika la mawasiliano ZICTIA na kampuni ya mtandao wa Simu TIGO-ZANTEL zimesaini Mkataba wa Makubaliano wa kupeleka huduma ya mtandao wa internet majumbani pamoja na kuweka kamera za CCTV katika baadhi ya maeneo visiwani Zanzibar
Makubaliano hayo yalioshuhudiwa na maafisa wa taasisi hizo yamefanyika huko katika ofisi ya wizara ya ujenzi, mawasiliano na Uchukuzi iliopo Kisauni Zanzibar.
Mkurugenzi mtendaji wa wakala wa miundombinu ya Tehama Shukuru Awadh Suleiman amesema makubaliano hayo yataongeza wigo wa matumizi ya internet kwa kwa kila mtu na kwa urahisi zaidi.
Amefahamisha kuwa huduma iliopo sasa imekuwa ni kwa watu wenye uwezo pekee na kunyima fursa Kwa watu wa kipato cha chini hivyo kufikiwa kwa makubaliano hayo yataenda kurahisisha huduma hiyo kutumika kwa Kila mwananchi mwenye uhitaji
Mkurugenzi huyo amesema kwa dunia ya sasa kuna kila sababu ya wananchi kirahisishiwa huduma ya internet ili kwenda sambamba na ulimwengu wa kidigital.
Amebainisha kuwa kwa sasa wataanza na maeneo ya mjini ikiwemo mji mkongwe na sasa wameanza kufanya utafiti kwa maeneo ya vijijini ili kujua namna ya kusogeza huduma hiyo kwa urahisi kwao.
Nae Mtendaji mkuu wa Kampuni ya Tigo-Zantel Kamal Okba amesema maamuzi yao ya kuiunga mkono serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi ni kutatua changamoto za huduma za Internet Zanzibar nzima.
Amesema mbali ya huduma ya internet majumbani pia wanampango wa kuweka camera zenye uwezo mkubwa barabarani ili kunusuru ajali za barabarani na kuhakikisha vyombo vya moto vyote vinafuata Sheria zilizowekwa.Makubaliano hayo yanatarajiwa kuanza na utafiti wa maeneo mbalimbali ya Zanzibar Kwa muda usiozidi miezi Saba 7 ya kujiandaa.
No comments: