Na Mwandishi Wetu
Shirika la Viwango Tanzania ( TBS) , jana Septemba 22,2023 katika Kijiji Cha Msomera Wilaya ya Handeni - Tanga limefanya Ukaguzi wa Bidhaa zilizopitwa na Wakati pamoja na kutoa Elimu kwa Wafanyabiashara na Wananchi juu ya Umuhimu wa kuzingatia muda wa matumizi ya bidhaa husika hasa za Chakula.
Aidha Maafisa wa TBS wamebaini na kuziondoa sokoni baadhi ya bidhaa hasa Za Vinywaji ambazo zimepitwa na wakati na kuwasisitiza wafanyabiashara kuzingatia muda wa matumizi ya bidhaa ikiwemo na kuhakikisha wanauza bidhaa bora.
Akizungumza katika eneo la Mnada wa Msomera baada ya kumaliza zoezi la kukagua na kutoa Elimu kwa Wananchi na Wafanyabiashara, Afisa Usalama Wa Chakula kutoka kanda ya Kaskazini TBS Bi. Mariam Maarufu amesema Shirika hilo limejipanga kuhakikisha linaondoa Bidhaa hafifu sokoni ikiwemo zilizopitwa na wakati ili kulinda afya za walaji.
" Leo tupo katika kijiji cha Msomera na tumeyafikia na kufanya ukaguzi katika maduka kadhaa ambapo tumebaini na kuziondoa Sokoni bidhaa ambazo zimepitwa na wakati lakini pia tumetoa elimu kwa wananchi kuhakikisha wanaangalia muda wa mwisho wa matumizi ya bidhaa ( expire date) kabla ya kuzinunua ili kuepukana na matatizo ya kiafya ambayo yanaweza kuwakumba kutokana na matumizi ya bidhaa zilizopitwa na wakati " amesema Bi Mariam
Nao kwa nyakati Tofauti Tofauti Simon Kipondo Mfanyabiashara Msomera na Martine Oleikayo Paraketi Mwenyekiti Wa serikali ya Kijiji Cha Msomera wamelipongeza shirika la Viwango Tanzania ( TBS ) kwa kuwakumbuka na kuja kufanya Ukaguzi pamoja na kutoa elimu maana imewafumbua mambo mengi hasa kuhusu matumizi ya bidhaa, Aidha wameliomba Shirika hilo kuongeza Elimu zaidi ili Kujenga uelewa zaidi kwa wananchi.
TBS WATUA MSOMERA , WAFANYA UKAGUZI WA BIDHAA ZILIZOISHA MUDA WA MATUMIZI SOKONI
Reviewed by Adery Masta
on
September 23, 2023
Rating:
No comments: