Header Ads Widget

Recent in Sports

test

ZAIDI YA WATEJA ELFU 13 WAMEJISHINDIA MAMILIONI YA PESA NA ZAWADI KIBAO KAMPENI YA " TIGO CHA WOTE" WIKI YA SITA

 Na Mwandishi Wetu. 

Ikiwa ni Takribani wiki sita sasa tangu kampuni ya Mawasiliano ya Tigo izindue Kampeni yake ya CHA WOTE yenye lengo la kuwasaidia wateja wa Tigo kutimiza malengo yao waliojiwekea ndani ya mwaka huu , ambapo wateja zaidi ya 320 kila siku wanajishindia zawadi mbalimbali kama vifurushi vya Dakika na MB na kubwa zaidi  Fedha Taslimu hadi Milioni tano kwa kufanya miamala tu kupitia TigoPesa.

Akizungumza Leo Agosti 4, 2023. Wakati wa Kuwakabidhi Mfano wa Hundi Baadhi ya Washindi wa Milioni Moja Moja wiki ya Sita,  Meneja wa Bidhaa Tigo Bwn. Eginga Mohamed amesema kuwa hadi sasa ikiwa ni wiki sita tu tangu Kampeni iyo izinduliwe wameshapatikana washindi zaidi ya Elfu 13 kutoka maeneo mbalimbali nchini .

" Leo tunayo furaha kubwa kuwa na baadhi ya washindi wa Wiki ya sita wa Kampeni yetu ya CHA WOTE ambao hawa ni washindi wa Milioni Moja Moja kila mmoja, Lakini niwakumbushe Watanzania kwamba kila siku tunatoa zawadi ikiwemo pesa taslimu hadi Milioni Moja kwa washindi 320 ,kuibuka mshindi ni rahisi tu unachotakiwa ni kufanya miamala na Tigo Pesa kama Kutumia Lipa Kwa Simu , Kununua Vifurushi , Kulipia Bili kwa Tigo Pesa , n.k kwa kufanya ivyo nawewe siku si nyingi utakua miongoni mwa Washindi wa Kampeni hii ya CHA WOTE ", na cha kufurahisha zaidi hii ni Kwa watumiaji wote wa Tigo Kwa maana ya kwamba hata mtu akisajili laini leo tiyari anauhakika wa kuwa Mshindi,  Alisema Eginga. 

Naye kwa Upande wake Mwajabu Omary Kiongozi mfanyabiashara ndogo ndogo mkazi wa Dar Es Salaam amesema kuwa ana furaha kubwa kuibuka mshindi wa Kampeni hii na hakutegemea kama hata Watanzania wenye kipato cha kawaida wanaweza kushinda

" Kwakweli nikiri nimefurahi sana jamani , Mimi ni Nafanya biashara ndogo ndogo na huwa nafanya miamala mbalimbali kama kulipia bili , na kununua Vifurushi vya SMS na Muda wa Maongezi nafikiri ivyo ndo vimenifanya nkawa mshindi , kwakweli hakika hiii ni CHA WOTE maana kumbe inawezekana kila mtu akawa , ushauri wangu ni kwamba tufanye miamala kwa wingi na TIGO PESA,  Na kununua muda wa maongezi maana ndo Siri Ya ushindi " amesema Bi.  Mwajabu


ZAIDI YA WATEJA ELFU 13 WAMEJISHINDIA MAMILIONI YA PESA NA ZAWADI KIBAO KAMPENI YA " TIGO CHA WOTE" WIKI YA SITA  ZAIDI  YA WATEJA ELFU 13 WAMEJISHINDIA MAMILIONI YA PESA NA ZAWADI KIBAO KAMPENI YA " TIGO CHA WOTE" WIKI YA SITA Reviewed by Adery Masta on August 04, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.