Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda amezitaka Taasisi za Elimu kutumia bunifu zao katika kuhakikisha zinawaingizia fedha ambazo zitasaidia kuendesha baadhi ya shughuli zao kwenye taasisi.
Waziri Mkenda ameyasema hayo jana Agosti 28,2023 Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa bodi ya Kampuni Tanzu ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) inayofahamika kama DIT Company.
Zipo bunifu Nyingi zinafanywa na watanzania katika secta mbalimbali lakiñi zimekua zikiishia kuwa vivutio kwenye maonesho pekee.
"Ifike mwisho hizi bunifu kuziona tu Kwenye Maonesho sasa nataka nialikwe kwa Maonesho ya bidhaa ambazo tunakwenda sokoni kama zile za Vipuri vya Bajaji" Amesema Waziri Mkenda.
Katika hatua Nyingine Prof. Mkenda amewataka wakufunzi wa tasisi za elimu kuwasaidia wabunifu ili kukidhi mahitaji ya soko kulingana na bunifu zao, "Wapo wafumbuzi wengi wanabidhaa Nyingi nzuri lakiñi hawana elimu au uelewa wa kuzigeuza vumbusi zao kuwa Biashara kwasababu wanakosa njia sahihi ya ujasiriamali, tuwasaidie"
Prof. Mkenda amehitimisha Kwa kuwataka watendaji wa tasisi hiyo kufikiria Zaidi ili kuanza kugeuza ubunifu wa teknolojia kuwa rasilimali ili kuongeza mapato ya tasisi na kutengeneza ajira Kwa watanzania.
WAZIRI MKENDA AZINDUA BODI YA KAMPUNI TANZU YA DIT
Reviewed by Adery Masta
on
August 29, 2023
Rating:
No comments: