Na Mwandishi Wetu.
Ikiwa ni Takribani wiki Tatu sasa tangu kampuni ya Mawasiliano ya Tigo izindue Kampeni yake ya CHA WOTE yenye lengo la kuwasaidia wateja wa Tigo kutimiza malengo yao waliojiwekea ndani ya mwaka huu , ambapo wateja zaidi ya 320 kila siku wanajishindia zawadi mbalimbali kama vifurushi vya Dakika na MB na kubwa zaidi Fedha Taslimu hadi Milioni tano kwa kufanya miamala tu kupitia TigoPesa.
Akizungumza Leo Julai 14, 2023. Wakati wa Kuwakabidhi Mfano wa Hundi Baadhi ya Washindi wa Milioni Moja Moja wiki ya Tatu , Balozi WA Promosheni Ya CHA WOTE na Mtangazaji Maarufu Nchini MILLARD AYO amesema kuwa hadi sasa ikiwa ni wiki Tatum tu tangu Kampeni iyo izinduliwe wameshapatikana washindi Takribani 6742 kutoka maeneo mbalimbali nchini ." Leo tunayo furaha kubwa kuwa na baadhi ya washindi wa Wiki ya Tatu wa Kampeni ya TIGO CHA WOTE ambao hawa ni washindi wa Milioni Moja Moja kila mmoja, Lakini niwakumbushe Watanzania kwamba kila siku CHA WOTE inatoa zawadi ikiwemo pesa taslimu hadi Milioni Moja kwa washindi 320 ,kuibuka mshindi ni rahisi tu unachotakiwa ni kufanya miamala na Tigo Pesa kama Kutumia Lipa Kwa Simu , Kununua Vifurushi , Kulipia Bili kwa Tigo Pesa , n.k kwa kufanya ivyo nawewe siku si nyingi utakua miongoni mwa Washindi wa Kampeni hii ya CHA WOTE ", kuwa na laini ya TIGO ni mchongo. " Alisema Millard Ayo." Kwakweli nikiri nimefurahi sana jamani , Mimi Nafanya biashara ya Mkapa na huwa nafanya miamala mbalimbali kama kulipia bili , na kununua Vifurushi vya SMS na Muda wa Maongezi nafikiri ivyo ndo vimenifanya nkawa mshindi , kwakweli hakika hiii ni CHA WOTE maana kumbe inawezekana kila mtu akawa mshindi hata sisi wenye kipato cha kawaida , katika maisha yangu Sikumbuki kama nilishawahi kushinda chochote, hii milioni moja inaenda kubadilisha Biashara Yangu hakika Tigo mnaenda kubadilisha maisha yangu" Alisema Restuta Muda mchache baada ya Kukabidhiwa Hundi yake ya Milioni Moja Makao Makuu ya Tigo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Washindi wengine wa Milioni Moja waliokabidhiwa Hundi zao Leo hii ni Kulwa Abdallah Mgogo ( 52 ) mkazi wa Kigamboni ,
Fatuma Khatibu (45) Msusi , Mkazi Buza Dar Es Salaam, Peter Mwasandumbe Fundi Gereji Mkazi wa Kurasini Dar Es Salaam.
No comments: