Na Mwandishi Wetu.
Meneja wa Uhusiano na Masoko Shirika la Viwango Tanzania ( TBS ) Bi. Gladness Kaseka amesema kuelekea msimu huu wa SabaSaba ambao utaanza rasmi tarehe 28/6/2023 hadi 13/7/2023 TBS wanatarajia kushiriki kivingine tofauti na walivyozoeleka miaka ya nyuma .
Akizungumza na Waandishi wa habari katika makao makuu ya Shirika hilo Jijini Dar Es Salaam Bi. Gladness amesema Licha ya kutoa huduma hapo kwa papo wanakuja kwa lengo la kuwawezesha wajasiriamali wadogo ambao watapewa huduma BURE kabisa wanachotakiwa kuwa nacho ni Barua kutoka SIDO, TIN NUMBER na LESENI YA BIASHARA
" Serikali huwa inatenga kiasi cha fedha kupitia TBS kuanzia million 100 hadi 200 kila mwaka kuhakikisha kwamba tunahudumia wajasiriamali wadogo na mwaka huu tutawatembelea kwenye mabanda yao ili kujua wale ambao hawajasajili mpaka sasa kwani huduma hiyo ni BURE" Amesema.
Kwa wale ambao wako nje ya mkoa wa DAR ES SALAAM watafanya utaratibu kujua ni jinsi gani ya kuweza kuwafikia na kuhakikisha bidhaa zote zinakuwa na ubora na chapa ya TBS au mteja anaweza kupiga simu namba ya BURE KABISA ya 0800110827.
Aidha Bi. Gladness amesema kuna bidhaa za vyakula na vipodozi kwa wale wanaotaka kusajili majengo ya vyakula na vipodozi basi huduma hiyo itapatikana kwenye msimu huu wa sabasaba unatakiwa kuwa na PICHA NA LESENI YA BIASHARA kwa sababu huduma za TBS zinapatika katika mfumo kama mtu ana tatizo la mfumo ataweza kupatiwa huduma
"Tutakuwa kwenye Banda la uwekezaji viwanda na biashara kuwapatia huduma hiyo kuanzia 28 - 13 katika viwanja vya sabasaba wateja pamoja na wananchi kwa ujumla tunawakalibisha kwenye Banda letu kuweza kujifunza na kutatuliwa changamoto mbalimbali karibuni Sana". Alimalizia
No comments: