Header Ads Widget

Recent in Sports

test

WATUMIAJI WA CHAKULA WAASWA KUZINGATIA MAELEKEZO YA UTUMIAJI SALAMA , KUELEKEA SIKU YA CHAKULA SALAMA DUNIANI


Kaimu Meneja Kitengo cha Tathmini ya Vihatarishi vya chakula TBS, Dkt.Ashura Kilewela akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 25,2023 , katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Chakula Salama ambayo hufanyika kila ifikapo tarehe 7 Juni kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni '' VIWANGO VYA CHAKULA HUOKOA MAISHA ".

KATIKA kuelekea Maadhimisho ya Chakula Salama Duniani Shirika la Viwango Tanzania (TBS)  limeitaka Jamii  kuzingatia kiwango kinachoelekeza kipimo cha chakula na ufungashaji na kuwasihi watumiaji wa vyakula kuzingatia maelekezo ya utumiaji wa chakula husika ambayo sana sana hupatikana katika vifungashio , hayo yameelezwa na Kaimu Meneja wa Kitengo cha Tathmini ya Vihatarishi vya Chakula Dkt. Ashura Kilewela wakati akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya TBS Jijini Dar Es Salaam 

AIDHA  kuelekea Maadhimisho hayo TBS inawakumbusha wananchi kutumia chakula salama hasa katika uzingatiaji kwenye uandaaji kwa kutumia malighafi safi pamoja na utunzaji wa chakula.


Maadhimisho hayo hufanyika kila ifikapo tarehe 7 Juni kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni 'Viwango vya Chakula Huokoa Maisha'.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 25,2023 Jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Kitengo cha Tathmini ya Viatarishi vya chakula TBS, Dkt.Ashura Kilewela amesema viwango vya uhakika huokoa maisha na ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku hivyo basi tuhakikishe tunatumia chakula salama kulinda afya zetu.

"Uandaaji wa chakula salama ni jukumu letu sote, kwahiyo ili tuwe na chakula salama kila mmoja anatakiwa kutumia kiwango vile inavyotakiwa ". Amesema

Amesema maadhimisho ya mwaka huu TBS inategemea kuwashirikisha wananchi na wadau mbalimbali katika kusheherekea maadhimisho hayo lengo kubwa ni kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa matumizi ya chakula salama.

"Lengo la maadhimisho haya ni kuinua uelewa wa jamii juu ya chakula salama kwasababu ukila chakula salama utakuwa na afya bora na utaweza kufanya majukumu yako ya kila siku". Amesema Dkt.Kilewela.

Hata hivyo amesema kuwa wanapoelimisha jamii wanasaidia kuepukana na madhara yanayopatikana na ulaji wa chakula kisicho salama.
WATUMIAJI WA CHAKULA WAASWA KUZINGATIA MAELEKEZO YA UTUMIAJI SALAMA , KUELEKEA SIKU YA CHAKULA SALAMA DUNIANI WATUMIAJI WA CHAKULA WAASWA KUZINGATIA MAELEKEZO YA UTUMIAJI SALAMA , KUELEKEA SIKU YA CHAKULA SALAMA DUNIANI Reviewed by Adery Masta on May 25, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.