Na Mwandishi Wetu
Mwanaharakati Huru Bihimba Mpaya amekabidhi mabati 40 kwa uongozi wa Msikiti AL - MASJID NUUR ISLAMIYA KIVULE uliopo Ukonga jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba vya Madrasa .
Akizungumza baada ya kukabidhi mabati hayo Mwanaharakati Bihimba amesema" Zaidi ya kuendelea kuwapongeza viongozi wa msikiti wetu huu , na ndio maana hata mimi leo Bihimba N. Mpaya , kijana wa kawaida wa mtaani nimekuja hapa kuwaunga mkono kwa kuleta mabati 40 , hii ni kwa sababu ninaona kazi nzuri wanayoifanya , hasa katika kuilinda na kuitetea dini yetu ya kiislam na kusisitiza maadili yaliyo mema kwa watoto wetu na katika jamii, mfano mzuri ni sakata hili la ushoga na usagaji ambalo limeshika hatamu katika nchi yetu hivi karibuni , nimekua nkiona Waislam kupitia nyie viongozi wetu kote nchini mkilipinga vikali kupitia mihadhara mbalimbali , kwakweli kwa hilo nawapongeza sana ."
Mimi kwa kushirikiana na wenzangu tutazidi kuwa nanyi na kuwaunga mkono popote penye changamoto , ili tu kwa lengo la kuitengenezea mazingira jamii na kizazi kinachokuja kuweza kuisoma na kuielewa dini yetu ya kiislamu. " Alimalizia Mwanaharakati Bihimba .Naye kwa upande wake Imam wa Msikiti AL - MASJID NUUR ISLAMIYA KIVULE Hussein Udenda amempongeza Mwanaharakati Bihimba kwa kusaidia katika masuala mbalimbali ya kijamii na kuongezea kuwa si leo tu maana alishawahi pia kutoa mifuko ya simenti msikitini hapo.
No comments: