Samwel Chanai-Meneja Mauzo wa Tigo Mkoa wa Iringa akiteta jambo na Mwangaza Matotola-Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja (TIGO) katika hafla ya iftar iliyoandaliwa na Tigo, Wilayani Tunduru kwaajili ya wateja wake, kushoto ni Laverty Khana-Meneja wa Tigo kanda ya Kusini.
Baadhi ya Wateja wa Tigo - Tunduru wakijipatia Iftari iliyoandaliwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo
Na Mwandishi Wetu
Kampuni namba moja nchini katika utoaji wa huduma za Kidigitali Tigo , Jumatano ya April , 19 imefuturisha Mawakala na wateja wake katika wilaya ya Tunduru Mkoani Iringa , Iftari iliyoudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa dini ya kiislamu , Mawakala , Wateja pamoja na wafanyakazi wa Tigo.
Akizungumza baada ya Iftari hiyo Samwel Chanai-Meneja Mauzo wa Tigo Mkoa wa Iringa amewashukuru wateja wa Tigo na Mawakala katika wilaya ya Tunduru kwa kukubali mualiko huo na kwa kutumia huduma za mtandao wa Tigo .
" Tigo kama ilivyo kawaida yetu kurudisha kwa jamii , na kwakweli leo tunatoa shukran zetu za dhati kwa wateja na Mawakala wetu wa wilaya hii ya Tunduru kwa kujumuika katika Iftar hii kwa maana kama ilivyo kawaida hasa katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan , Mwezi wa rehema na baraka uwajumuisha na kuwaunganisha watu pamoja , na ndio maana sisi kama Tigo tumeamua tukutane na Wateja Wetu si tu Wilaya hii ya Tunduru bali na maeneo Mengine bara na visiwani , Kwakweli tunashukuru sana na niwatakie mfungo Mwema "Alimalizia Bwn. Chanai.
No comments: