Mkurugenzi wa Biashara kutoka Shirika la PASS TRUST akizungumza na Wakulima katika mkutano maalum uliolenga kuwaendeleza na kuwaunganisha Wakulima kuwaunganisha na Huduma za Kifedha ili waweze kulima kibiashara zaidi , hapo Jana Mjini Babati.
Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange akizungumza na Wakulima pamoja na Wadau wa Kilimo PASS TRUST katika mkutano Maalum ulioandaliwa na PASS TRUST .
Baadhi ya Wakulima , walioshiriki Mkutano Maalum ulioandaliwa na Shirika la PASS TRUST , Lengo likiwa ni kuwaendeleza na kuwaunganisha Wakulima kuwaunganisha na Huduma za Kifedha ili waweze kulima kibiashara zaidi , hapo Jana Mjini Babati.
Na Mwandishi Wetu.
Zaidi ya wakulima Milioni tatu kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania wamenufaika na fursa mikopo ya kilimo biashara iliyowawezesha kulima kwa tija na kuuza mazao yao katika masoko ya ndani na nje ya nchi hivyo kuongeza kipato chao .
Shirika la kilimo la PASS TRUST likizungumza na wakulima limeahidi kuendelea kuwawezesha wakulima kwa kuwaunganisha na huduma za kifedha ili waweze kulima kibiashara zaidi .
Naye Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe . Lazaro Twange amesema serikali itaendelea kushirikiana na wadau katika kuboresha sekta ya kilimo nchini .
Aidha wakulima mkoani Babati wamepongeza juhudi za wadau wa Kilimo hasa Shirika la PASS TRUST katika kuhakikisha wakulima wanakopesheka.
No comments: