BENKI YA EQUITY YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE KWA KIPAUMBELE CHA SULUHISHO ZA KIDIGITALI KATIKA HUDUMA ZAO ZA BENKI
Benki ya Equity inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa kipaumbele cha suluhisho za kidigitali katika huduma zao za benki kwa wanawake. Kauli mbiu ya kimataifa ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake ya mwaka huu ni “Ubunifu na Teknolojia zinatumika kufikia Usawa wa Kijinsia”.
Mapema mwaka huu, Benki ya Equity ilizindua kampeni yao mpya iliyoitwa “TUMERAHISHA” kwa lengo la kuwafanya wateja wao waweze kupata huduma za benki za kidigitali kwa urahisi zaidi. Ili kurahisisha huduma za benki kwa wanawake, wameanzisha mikopo ya kidigitali ambayo inaondoa haja ya kwenda benki kimwili kupata mikopo. Wamiliki wa akaunti za kikundi pia wanaweza sasa kupata huduma zao kupitia simu zao za mkononi. Aidha, wanatoa mikopo ya kilimo kusaidia wanawake katika kuboresha kilimo chao na kugeuza kuwa biashara yenye faida ili kujiunga kiuchumi.
Mwaka huu, lengo kuu ni kusherehekea wanawake na wasichana ambao wamebadilisha teknolojia katika sekta mbalimbali, ikiwemo benki, kote ulimwenguni. Benki ya Equity iko mstari wa mbele katika mapambano ya kuhakikisha huduma zao zote zinadigitilizwa. Wanajivunia kuwa na Mkurugenzi Mtendaji mwanamke, ambayo ni hatua kubwa kwao kama taasisi kuonyesha kwamba wanawake wanaweza kuongoza kwa mifano halisi.
Ni muhimu kuendelea kupigania usawa wa kijinsia wenye manufaa. Kwa muda mrefu, wanawake wameachwa nyuma katika ushiriki wa teknolojia. Tunapaswa kuongeza ushiriki wa wanawake katika teknolojia kwa sababu maendeleo hayawezi kutenganishwa na teknolojia. Benki ya Equity inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake siyo tu kwa kutambua mafanikio ya wanawake bali pia kwa kutoa elimu ya kidigitali kwenye majukwaa mbalimbali.
No comments: