Na Mwandishi Wetu.
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewataka ,Waagizaji na Wasambazaji wa Maziwa mbadala ya watoto wachanga na wadogo kuhakikisha bidhaa hizo zinasajiliwa kwa mujibu wa sheria ya Viwango na Shirika hilo ili kuhakiki ubora na usalama wa bidhaa hizo kabla hazijamfikia mtumiaji.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Februari 17,2023 Jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Ukaguzi na Utekelezaji wa Sheria TBS, Bw. Mosses Mbambe amesema wale wote ambao wanaoagiza bidhaa za maziwa mbadala ya watoto wadogo wanatakiwa kuyasajili ili kuangalia ubora na usalama kwamujibu wa viwango vya kitaifa.
Amesema katika usajili wanaangalia pia maelezo ya kwenye lebo ama kwenye vifungashio kama yameelezwa kwa usahihi kwa lengo la kutoa taarifa sahihi kwa mama ambao wameamua kutumia bidhaa hizo.
"Kwa mujibu wa kanuni chini ya sheria ya viwango sura ya 130 inataka maelezo ya kwenye lebo ya maziwa ya watoto wachanga na wadogo yawe katika lugha ya kiswahili kwasababu ni lugha ambayo inaeleweka na watanzania waliowengi na itamuwezesha mama ambaye amefanya maamuzi ya kutumia bidhaa hiyo namna ya kuyaandaa vizuri mwa usahihi kwa lengo la kuepuka athari ambazo zinaweza kujitokeza". Amesema Bw.Mbambe
Aidha Bw.Mbambe amesema kwa mujibu wa kanuni ama sheria ya kimataifa maziwa hayo ya watoto wachanga na wadogo hayaruhusiwi kutangazwa katika maeneo mbalimbali nchini lengo kubwa ni kuhakikisha kwamba wanahamasisha uyonyeshaji wa maziwa ya mama kwa watoto.
TBS YAWATAKA WAAGIZAJI WA MAZIWA MBADALA YA WATOTO KUHAKIKISHA WANASAJILIWA
Reviewed by Adery Masta
on
February 17, 2023
Rating:
No comments: