Bi. Kimaryo anachukua nafasi hiyo kufuatia kustaafu kwa Bw. Ernest S. Massawe ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi kwa miaka kumi iliyopita ambapo aliweza kutoa mchango mkubwa katika ukuaji na maendeleo ya Benki ya ACB kwa ujumla. Chini ya uongozi wake thabiti, Bodi na Menejimenti ilifanikiwa kukabiliana na nyakati zenye changamoto ikiwa ni pamoja na janga la kimataifa la UVIKO-19.
Mwenyekiti wa Bodi (Bi. Kimaryo) analeta hazina kubwa ya maarifa kufuatia uzoefu wa miaka zaidi ya 20 katika sekta ya fed ha hususan taasisi za kibenki na uwekezaji kwenye nchi na masoko yanayoibukia barani Afrika na katika bara nyingine kadhaa.
uongozi na utawala. Mbali na Bodi ya ACB, Bi. Kimaryo anahudumu kama Mkurugenzi katika bodi nyinginezo ndani na njeya nchi. Kwa ujumla, Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya ACB inampongeza Bi. Kimaryo na inategemea kutumia hazina kubwa ya maarifa, utalaamu, uzoefu, ari na weledi wa Mwenyekiti wao mpya kutimiza maono na mkakati wa Benki unaongozwa na agenda kuu ya mabadiliko. Bi. Kimaryo ana Diploma ya Juu ya Utawala (INSEAD, Ufaransa); Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara (Wits Business School, Afrika Kusini); na Shahada ya Kwanza ya Biashara (Chuo Kikuu cha McGill, Canada).
Aidha, Bi. Kimaryo pia ni mzungumzaji wa umma aliyebobea, mshauri, msimamizi na mwendeshaji mijadala mbali mbali hasa katika tasnia ya fedha.
No comments: