Meneja wa Uber Kanda ya Afrika Mashariki Bwn. Imran Manji amesema " Tuna furaha sana kurudi na kuendelea kutoa huduma zetu za usafiri nchini Tanzania na tunaipongeza serikali kwa juhudi zake za kukuza huduma za usafiri wa Teksi kupitia mtandaoni , kipaumbele chetu ni kuwa na mfumo ambao utawasaidia madereva kutengeneza kipato cha kujikimu sambamba na kutoa usafiri wa uhakika na wa kutengemewa kwa Watanzania "
Kampuni ya Uber imerudisha huduma za UberX na UberXL ambazo wasafiri wanaweza kutumia katika jiji la Dar Es Salaam , Uber X ni huduma ya bei nafuu ambayo inawawezesha watu wengi kufurahia huduma za usafiri wa uhakika kwenye mfumo wa UBER , Huduma za Uber XL kwa ajili ya Wasafiri sita na magari yanayotoa huduma hii yana nafasi inayotoa usafiri wa starehe na huduma hii inafaa kwa safari za familia , marafiki au msafiri anaposafiri akiwa na mizigo mingi .
Sekta ya usafiri wa teksi za mtandaoni imeleta mageuzi makubwa katika namna watu wanavyosafiri katika miji yetu na tangu mwaka 2016 UBER ilipoanza kutoa huduma zake jijini Dar Es Salaam kampuni ya uber imekua mshirika muhimu katika jiji hili kwa kutoa usafiri wa kutumia teknolojia ya kisasa , kuchangia katika huduma xa kiuchumi , kuwapa madereva uhuru wa kufanya kazi kwa muda wanaoutaka sambamba na ulipaji kodi .
Uber imeweka.msukumo mkubwa kwenye usalama ,na kadri watu wanavyoendelea kutumia teksi za mtandaoni ndivyo UBER itaendelea kuwekeza kwenye usalama , kwa mujibu wa utafiti uliofanywa raia wengi hawana uelewa wa vipengele vya usalama ambavyo wanaweza kuvitumia wanapokua safarini Hivyo basi Uber imeanzisha kampeni inayohamasisha kuhusu usalama maarufu kama SAFETY CHECK UP nchini Tanzania ambayo inalenga kuimiza wasafiri kukamilisha safari zao kwa usalama , kuwasha na kutumia vipengele vya usalama vinavyopatikana kwenye mfumo wetu kama vile Watu unaowaamini , Uthibishaji wa PIN na kukagua taarifa za gari na dereva yaan RIDE CHECK .
Imran amehitimisha kwa kusema " Bila shaka tuna matarajio makubwa kuhusu kesho ya soko la Tanzania , Tupo tayari kushirikiana na watunga sera , kuimarisha usalama , kusaidia madereva kukuza biashara yao sambamba na kuboresha huduma kwa abiria wanaotumia mfumo wetu.
No comments: