Na Mwandishi Wetu
Siku ya Alhamisi 27 Oktoba 2022, Benki ya I&M Tanzania hivi karibuni imefanya hafla ya chakula cha jioni na wateja wake iliyofuatiwa na usiku wenye muziki na burudani katika ukumbi wa Serena Hotel, Dar es salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa Benki ya I&M Tanzania Ltd bwana Zahid Mustafa alifungua hafla kwa kutambua uwepo wa wafanyakazi mbalimbali wa Benki ya I&M ambao kupitia kufanya kazi kwa bidii na utayari wao wameendelea kutoa huduma za kiwango cha kipekee ambacho kinaitambulisha benki na kuwashukuru wateja kwa kuendelea kuwaunga mkono.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji (CEO), “Nina furaha kusema kwamba Benki ya I&M ni miongoni mwa benki chache ambazo zimeendelea kuwa imara na kukua kwa kuongeza idadi ya wateja wake, amana (fedha zilizowekwa), pamoja na jumla ya mali. Vile vile ninauhakika kusema kwamba benki hii itaendelea kutekelea mikakati yake ya kibiashara na kuhakikisha kwamba inaendeleza kasi ya mwenendo wa ukuaji kama ambavyo tumetambulisha huduma mpya inayoitwa “Select Banking” Tuna kitengo maalumu cha huduma ya Select Banking katika tawi la Oysterbay, Tawi Kuu, na Kitengo cha Select Banking cha aina yake katika tawi letu la Arusha kwaajili ya kuhudumia mtindo wako wa Maisha wa kipekee na mahitaji ya kifedha.”
Aliendelea kufafanua kwamba, “Huduma mpya inajumuisha faida kadhaa za kipekee, ikiwemo nafasi ya kutumia maeneo ya mapumziko katika viwanja vya ndege zaidi ya 1,200 duniani kote, pamoja na kutumia hotel za kifahari za Visa kama vile Peninsula, na Park Hyatt miongoni mwa nyingine nyingi. Kadi zetu za Visa Infinite na Platinum zenye ubora wa kiwango cha juu inakupatia bima kama vile bima ya safari ikiwemo bima ya Uviko 19 pamoja na ofa ya punguzo la bei kwa wafanyabiashara mbalimbali kufuatia utaratibu wa ushirikiano iliopo kati ya watoa huduma wa ndani na wale wa kimataifa ikiwemo hotel na migawaha, mashirika ya ndege na maduka ya chakula.”
Aliongezea kwamba, “tumetambulisha “I&M Bancassurance.” Sasa benki ya I&M ni taasisi ya kifedha yenye huduma kamilifu ambayo inaelewa vyema mahitaji ya kibenki ya wateja wake. Tumeweka mahitaji ya wateja wetu kuwa kipaumbele chetu katika uvumbuzi wetu wotekwa kuhakikisha kwamba tunakidhi mahitaji ya bima ya wateja wetu na kuhakikisha kwamba wamepatiwa elimu ya kutosheleza kuhusiana na bima. Benki ya I&M bado inafanya vizuri wenye huduma za “Utunzaji wa mali na Uwekezaji” "Custodial and Investment services" wakati ambapo tumepanua huduma zetu katika nchi za Mashariki na SADC. Benki ya I&M ni benki jumuishi ambayo inahudumia wateja wote katika ngazi zote, n ani kwa Msingi huu ambapo benki inazindua huduma ya mikopo ya kidigitali, inayojulikana kama “Kamilisha”
Mwenyekiti wa Bodi wa kampuni Bwana Sarit Shah akiwa katika hafla hiyo alisema, “Kundi la makampuni la Banki ya I&M Group PLC imedumisha mwenendo wa ukuaji wake katika sehemu ya kwanza mwaka 2022, ambapo kundi lilitoa taarifa ya ukuaji wa asilimia 16% katika faida baada ya kodi kwa Kes bilioni 4.9 ukilinganisha na Kes bilioni 4.2 katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2021. Kampuni zake tanzu zimekuwa zikidumisha utendaji wa kiwango cha juu kufuatia msaada na uungwaji mkono usiopimika kutoka kwenye huduma za wateja wakubwa (Corporate) wateja wadogo na wateja maalumu Pamoja na huduma zingine za kifedha zinazohusiana na kwamba Tanzania inabakia kuwa moja kati ya kampuni tanzu muhimu kutokana na fursa ambazo zinaweza kupatikana nchini.”
Mkurugenzi wa kanda wa Benki ya I&M (T) LTD bwana Chris Low alisema kwamna, “ Ninaweza kutoa uthibitisho katika mabadiliko makubwa yaliyotokea katika kanda, zaidi yah apo kama kundi tuna fursa ya mazingira ya kuleta maendeleo katika shughuli za kiuchumi; hivyo kwa namna Fulani kuweza kuchangia katika kasi ya ukuaji wa uchumi inayohitajika kwaajili ya kusafari ya kufikia mafanikio makuba. Matarajio ya mkakati wa kundi ni “Kuwa kampuni yenye nguvu ya kibenki katika Afrika Mashariki kwa biashara za kati na kubwa na wateja maalumu” tukitekeleza dhamira yetu kama mshirika wa ukuaji kwa wadau wetu wote.
I&M BENKI WATANGAZA NEEMA KWA WATEJA WAKE , WAKUTANA NA BODI YA WAKURUGENZI
Reviewed by Adery Masta
on
November 04, 2022
Rating:
No comments: