Washiriki wa mashindano ya Ubunifu katika sekta ya TEHAMA maarufu kama First Global Challenge katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye ( wa mwisho kulia ni Mkufunzi kutoka APPS & GIRLS Bwn. Raymond Luanda )
MMOJA wa wanafunzi wanaounda timu ya Apps & Girls, Maria Mtega (katikati) akitoa maelekezo mbele ya Waziri Nape, jinsi roboti maalumu inavyofanya kazi katika kukabiliana na ongezeko la hewa ya ukaa.
.............................................
Na Mwandishi Wetu
Kampuni namba Moja kwa utoaji wa huduma kidigitali hapa nchini Tigo Tanzania imeidhamini Taasisi isiyo ya kiserikali ya APPS AND GIRLS kwenda kushiriki mashindano ya Ubunifu katika sekta ya TEHAMA maarufu kama FIRST GLOBAL ROBOTICS CHALLENGE ambayo kwa mwaka huu 2022 yamefanyika nchini USWISI ambapo Tanzania iliibuka kidedea kwa kupata nafasi ya pili katika mashindano hayo.
Akizungumza baada ya Wasichana hao watano walioshiriki Mashindano hayo kufika ofisini kwake Waziri Nape amewapongeza kwa kuiheshimisha Tanzania kimataifa
" Takwimu mbalimbali za dunia zinaonesha ushiriki wa mabinti kwenye shughuli mbalimbali za TEHAMA sio mkubwa Sana kwahiyo unahitaji kampeni kubwa , kwahiyo hiki walichokifanya Hawa mabinti zetu ni mfano mzuri na umetuonyesha kwamba wakishiriki wanaweza kama wameweza kwenda duniani , wakishiriki na wakashinda maana yake ni kwamba mabinti wanaweza kufanya vizuri kuliko hata vijana wa kiume "
Aidha waziri Nape ameipongeza kampuni ya Mawasiliano ya Tigo kwa udhamini wao ambao umewawezesha Hawa wasichana kwenda katika mashindano hayo na kuibuka na ushindi wa nafasi ya pili .
Naye kwa upande wake Afisa Mkuu Udhibiti wa Tigo Bi. Sylvia Balwire amesema kuwa Lengo la kuwakusanya wasichana hao kupitia Apps & Girls na kushiriki mashindano ya Ubunifu ni kuongeza idadi ya Waandisi wa Teknolojia wanawake ili kupata wataalam wa Sayansi na Teknolojia .
" Tigo katika kuhakikisha kwamba masuala ya TEHAMA hatubaki nyuma na tunataka tuhakikishe tunashiriki kikamilifu kwenye mapinduzi ya nne ya Viwanda , tunashirikiana na APPS AND GIRLS kuhakikisha kwamba TEHAMA katika mashule hususani kwa watoto wa kike inathaminiwa na inachukuliwa Kama SoMo la msingi . Alimalizia
No comments: